kwamamaza 7

APR FC yaichapa Espoir na kushinda kombe la “Peace Cup”.

0

Katika mechi ya fainali ya Kombe la Amani “Peace Cup”  APR, timu ya majeshi wa Rwanda, imeweza kuwashinda Epoir ya wilaya ya Rusizi 1-0  na kunyakua ubingwa.

Ni katika mechi ambayo ilipigwa uwanja wa Kigali “Stade de Kigali” ambako APR iliwahi kushinda Espoir 1-0 kupitia mchezaji wake Bizimana Muhadjiri . Goli hilo ambalo lilipatikana dakika ya 38 ndilo lilofaa kuwawezesha APR kunyakua kombe hilo.

APR inashinda kombe hili kwa mara ya 9 na imefuzu tiketi ya kuwakilisha Rwanda katika mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika . APR pia ndio timu pekee ambayo imeweza kushinda ubingwa huu mara nyingi kuliko timu nyingine yoyote.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mechi hii ilishuhudiwa na mashabiki chungu nzima wengi wakiwa wa APR FC na wengine wa Rayon Sports mahasimu wao ambao walikuwa wakishabikia timu ya Espoir. Kulikuwa pia na viongozi wengine wakuu na hata majeshi akiwemo pia Waziri wa Ulinzi James Kabarebe ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa Heshma wa timu ya APR FC.

Na katika mechi ya kuwania nafasi ya tatu iliyopigwa awali Rayon Sports waliweza kuwapiga Amagaju Fc bao 3-0 na kuchukua nafasi ya tatu katika mashindano haya ya Kombe la Amani “Peace Cup”

APR ambao wametwaa ubingwa, licha ya ubingwa wamepewa pia milioni kumi za faranga za Rwanda(10,000,000) na Espoir ya pili ikapewa 3,000,000 huku Rayon Sports ya tatu na Amagaju FC ambayo ilishika nafasi ya nne zikipewa milioni 1,000,000 kila yeyote.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.