Swahili
Home » APR FC kuikuta Espoir iliyowatoa mahasimu wao Rayon Sports kwenye fainali ya “Peace Cup”
HABARI MICHEZO

APR FC kuikuta Espoir iliyowatoa mahasimu wao Rayon Sports kwenye fainali ya “Peace Cup”

Hatimaye APR FC yaitoa Amagaju FC na kuendelea kwenye fainali ya Kombe la Amani “Peace Cup” na wataikabili Espoir FC iliyowatoa Rayon Sport Mabingwa wa Rwanda.

APR FC imepata tiketi hii baada ya kuwalaza Amagaju FC kwa mabao 5 kwa nunge katika mechi yao ya pili ambapo mechi ya kwanza ilikuwa ni sare ya 1-1. Hapa APR walikuwa wanajuwa kwamba matumaini yao ya kuwakilisha nchi katika mashindano ya Kimataifa yanabakia tu kwa kushinda Kombe la Amani “Peace Cup”

Washindi wa bao hayo walikuwa ni Muhadjili, Bizimana Djihad 2 ,Sekamana Maxime,Nshuti Innocent. Na jumla ya matokeo 6-1 kwenye mechi mbili.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Espoir nayo ikiwa inalenga kuzifikia ndoto zake iliwatoa Rayon Sports baada ya mabingwa hawa wa Rwanda kushindwa kufunga magoli mawili ambayo walifungwa kwenye mechi ya kwanza walipokuwa mjini Rusizi wa jimbo la magharibi.

Espoir iwapo wataweza kuilaza APR kama walivyoifanyia Rayon Sport, wachukuwa kombe hili kwa mara ya kwanza na likifuatana na mamiliyoni ya fedha. Na zaidi ya kombe Timu ambayo itaibuka mshindi wa mechi hii itakuwa na tiketi ya moja kwa moja kuiwakilisha nchi katika kombe la shirikisho la CAF. Na ni bahati mbaya kwa Polisi FC ambayo ilikuwa ya pili katika liga ya nyumbani hapo wangetarajia Rayon Sport kutwaa kombe hili.

Fainali itapigwa tarehe 4Julai kwenye Stade de Kigali.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com