Swahili
Home » Amiri (Cpt) wa jeshi la Congo ameuawa
HABARI

Amiri (Cpt) wa jeshi la Congo ameuawa

Katika wilaya ya Ituri sehemu ya Ariwara, askari jeshi wawili wa DRC, walivamiwa na watu wenye silaha tarehe 4 Februari 2017 wakawauwa.

Capt Carlos Kalombo, msemaji wa jeshi la Congo FARDC amesema ya kuwa wahusika na shambulio hilo la Ituri hawajajulikana.

Aliendelea na kusema ya kuwa watu tatu walikuja na kuingia katika nyumba ambayo ilikuwa ndani wana jeshi wawili (sergent na capitaine) wakawapiga risasi na wakatoka wakaendea pikipiki ya wanajeshi hao waliouawa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Taarifa kutoka radio Okapi, husema pia kuwa waliiba pikipiki hio na chombo cha habari cha askari hao.

Baada ya siku moja ya upelelezi, uongozi wa jeshi la Congo wametangaza ya kuwa wamepata pikipiki  na vifaa vingine vilivyo ibwa.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com