kwamamaza 7

Aliyekuwa Kiongozi wa walinzi wa Rais Kagame alalamikia kufungiwa karantini

0

Aliyekuwa Kiongozi wa walinzi wa Rais Kagame, Kanali Tom Byabagamba ameweka wazi  alifungiwa karantini kinyume na uamuzi wa mahakama ya Kijeshi.

Mwaka 2016, koti iliamua kumfunga miaka 21 Kanali Byabagamba kwa kuwa na hatia ya kuhatarisha usalama wa nchi, kusambaza fununu, kuipaka masizi serikali na kudaharau bendera la nchi.

Jumatano,  mwanasheria wake, Me Gakunzi Valerie amesema mteja wake amefungiwa miaka mitatu karantini kinyume na uamuzi wa mahakama mwaka 2016.

“ Kumfunga mahari ambapo hakutani na watu wengine ni kumtesa kimwili.” Me Gakunzi amesema

Gakunzi ameitaka mahakama kumuachia huru mpito Kanali Byabagamba ili kutoa suluhisho kwa hili suala.

Kwa hilo, mahakama imemruhusu Byabagamba kufungiwa pamoja na wengine.

Mwendeshamashtaka amesema  rufaa yake Byabagamba ipigwe marufuku kwani ameipiga baada ya mwaka.

Byabagamba amefichua ametimiza miaka mitatu bila kutembelewa na mtu yeyote  hata wanafamilia yake.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.