kwamamaza 7

Akamatwa kwa madai ya uwizi wa bendera

0

Shirika za usalama wilayani Ngoma zimepiga jela Niyigena Methode kwa mashtaki ya kuiba bendera katika kiini cha Mvumba katani Murama. Methode mwenye umri wa miaka 27 anadaiwa kuiba bendera jana 27 Oktoba 2016.

Habari zinasema kwamba walinzi wa usalama walifika kazini jana 9h00 za jioni wakakosa bendera.

Buhiga Josué ambaye ni Kiongozi wa kata ya Murama alithibitisha habari. Aliambia gazeti la Imvaho Nshya kwamba bendera kutoka kata ya Mvumba imekosekana na mtuhumiwa amepigwa jela. Alisema kwamba kuna raia walimuona akizururazurura karibu na ofisi ya kata.

[ad id=”72″]

Alisema, “Bendera imekosekana. Tumeisha fanya mkutano na raia wote, anayedaiwa ni Niyigena Methode kutoka kijiji cha Rugarama. Anajulikana kwa kunyanganya na kutumia dawa za kulevya. Kuna raia mmoja aliyethibitisha kwamba alimuona karibu na bendera na alipomuuliza anachofanya alisema (Niyigena Mithode) kwamba ameachia mali yake hapo.”

Baada ya kukosa bendera, walipomtafuta Methode alikimbia kabla ya kumuambia kesi na kukimbilia mwituni; alipogunduliwa na shirika za usalama.

[ad id=”72″]

Niyigena Methode amefungiwa katika kituo cha polisi cha Kibungo, anakataa madai. Walinzi wa usalama wameamrishwa kuanza zamu saa kumi na mbili jioni badala ya saa tatu za jioni.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.