Swahili
Home » Afrika si jalala la magari makukuu- Rais Kagame
HABARI MPYA

Afrika si jalala la magari makukuu- Rais Kagame

Rais Kagame jana amesema   Afrika haistahili kuwa jalala la magari makukuu.

Rais Kagame  ametangaza haya akianzisha operesheni za Kiwanda cha Volkswagen(vw) nchini Rwanda.

“ Afrika haitaki kuwa jalala la magari yaliyozeeeka ama kifaa kingine kilichotumiwa mahali pengine” Kagame  amesema

“Ikiwa unalipa bei ghali kwa kununua kifaa kilichotumiwa kwa nini huwezi kunua kifaa mpya? Afrika na Rwanda wanahitaji mambo mazuri na hili ni mmoja ya namna ya kuonyesha kwamba tuna uwezo wa kufanya hili” ameongeza

Rais Kagame amesisitiza VW itafaidika kwa kuwa Wanafrika ni miongoni mwa wanaonunua mambo mengi duniani.

Mkurugenzi wa VW nchini AfriKA Kusini, Thomas Schafer amesema kwa nini walichagua kuanzisha opersheni zao nchini Rwanda

“Kuna mambo yaliyotusukuma kuja nchini Rwanda:kuna siasa yenye muelekeo,kupambana na rushwa,msimamo wa maendeleo ya uchumi na wakazi wenye umri mdogo wenye uwezo wa kutumia tekonolojia” Schafer ametetea

Inatarajika kwamba VW itawapa kazi watu karibu 1000.

Nchini Rwanda VW itaandaliwa magari  5000 ya aina ya VW Polo, VW Passat, VW Tiguan, VW Teramont na VW Amarok.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com