kwamamaza 7

Afrika Kusini kujiondoa mahakama ya ICC baada ya Tukio la Bashir

0

Afrika Kusini imeanzisha mchakato wa kujiondoa kutoka uanachama wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita yaani ICC baada ya shinikizo ilikumbana nazo mwaka uliopita za kuitaka imkamate rais wa Sudan Omar al Bashir wakati wa mkutano wa muungano wa nchi za Afrika mjini Johannesburg.

Wanadiplomasia wa Afrika kusini wamearifu umoja wa mataifa juu ya uamuzi huo na kuilaumu ICC kwa kuzilenga zaidi nchi za Afrika.

Septemba mwaka jana, mahakama nchini Afrika Kusini iliinyima serikali ya nchi hiyo ruhusa ya kukata rufaa uamuzi ulioishutumu kwa kukosa kumkamata rais Bashir alipohudhuria kongamano hilo mwezi Juni mwaka 2015.

[ad id=”72″]

Serikali ilitaka kukata rufaa uamuzi wa Mahakama Kuu ikisema Bashir alikuwa na kinga ya urais kwa sababu yeye ni kiongozi wa taifa.

Lakini Jaji Hans Fabricius alisema rufaa hiyo haiwezi kufanikisha chochote.

Aliongeza kuwa Afrika Kusini ni mwanachama wa Mkataba wa Roma uliounda mahakama hiyo, na kwamba mkataba huo unabatilisha sheria zozote ambazo huenda zingempa kinga Bashir asikamatwe na kushtakiwa.

[ad id=”72″]

Rais wa Sudan omar Hassan al-Bashir amekuwa akisakwa na Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kwa tuhuma za kutekeleza mauaji ya halaiki na makosa ya uhalifu wa kivita Darfur.

@Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.