kwamamaza 7

AERG/GAERG Week 2017: Watajenga nyumba 11 na 15 kujengwa upya

0

Wijana wa jamii ya wanafunzi walionusurika mauaji ya Kimbari dhidi ya watusi mwaka 1994 (AERG), pamoja na wakubwa zao wenye kuwa katika jamii ya GAERG, walianza kitendo cha kuwajengea wasio jiweza kama vile hufanywa kila mwaka “AERG/GAERG Week”, na watajenga nyumba 11 na kujenga tena upya 15.

Tendo hilo lilianzia katika wilaya ya Nyaruguru wakiwa na lengo la kutia nguvu nafasi moja kama vijana walio nusurika mauaji ya Kimabri ili kusaidiana na nchi kwa kuwasaidia wanusurika wa mauaji ya Kimbari dhidi ya  Watusi wenye kuwa na nguvu chache katika jamii ya Rwanda kwa ujumla. Wakati huu tunajiandaa tendo la kuwakumbuka na kuzingatia neno “kuokolewa hunikumbusha shukrani”.

Kwa kuanza AERG/GAERG Week 2017, vijana hao walijenga upya nyumba mbili katika kijiji cha Ruhunga, kiini cha Gorwe, tarafa la Nyaruguru.

Twahirwa Emmanuel, kiongozi  mkuu wa GAERG, alisema ya kuwa wanafanya hivi kwa ajili ya kutoa msaada kwa kutatua swala moja moja ambazo huwasumbua walio nusurika mauaji ya Kimbari dhidi ya Watusi.

Mukarugomwa Bernadette, aliye jengewa nyumba yake upya, alisema ya kuwa yeye na mume wake pamaoja na mtoto yatima wanao mulea waliishi miaka tatu wakinyeshewa na mvua, kwa kuwa mabati yalitwaliwa na upepo wakati wa mvua, anafurahia kuishi tena katika nyumba nzuri kama vile husema imvahonshya.

Mambo mengine inatarajiwa kama vijana hao kupana ng’ombe 11 na kupana kinga kwa wamoja walio patwa na shida wakati kupambana kwa kukomboa nchi. Baada ya wilaya ya Nyaruguru, wataendelea katika wilaya ya Rubavu, Ruhango, Kicukiro na Nyagatare, na watafikia mwisho wa tendo hilo tarehe 1 April 2017.

Tangu AERG/GAERG Week kuanza mwaka wa 2015, kwa ujumla wamejenga nyumba 17, wakajenga upya nyumba 12, na kusafisha kumbukumbu za ukumbusho 65, wakalima bustani ya jikoni 217, wakapana ng’ombe 21 na barabara ya urefu wa kilometa 13 ikasafishwa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com,

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.