Lori yenye mwendo wa kasi kwa mujibu wa mashahidi imewaangukia wasafiri mjini Kigali, eneo la Masizi, Wilayani Gasabo.

Wawili waliokuwa ndani ya lori wamejeruhiwa sana na mwendeshabasikeli mmoja amepatikana mahututi.

Mashahidi wamesema kuwa ajali imetokea mahali kwenye watu wengi na hawajui idadi ya walioangukiwa na lori.

Msemaji wa Polisi ya Barabarani, SSP Jean Marie  Ndushabandi amesema watu wawili wamejeruhiwa hapo hapo , halafu wakapelekwa hospitalini.

Imeripotiwa kwamba dereva wa lori amekimbia kisigino kisogoni baada ya ajali.

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.