kwamamaza 7

Rutsiro : Raia wanahitaji hospitali ya pili ili waweze kupata huduma za afya kwa urahisi

0

Upatikanaji wa huduma za afya siyo rahisi kwa wakazi wa wilaya ya Rutsiro kwa kuwa hali ya kijiografia inayofanya watu kutosafiri kwa urahisi. Na kwa hivyo raia wa Rutsiro wangependa mgombea atakayechaguliwa kuwa rais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi ujao kuweka mipangoni mwake kuwajengea hospitali ya pili ili ije ikawasaidia kupata huduma hizo.

Wilaya ya Rutsiro ina hadi sasa hospitali moja ya kiwango cha wilaya. Kulingana na hali yake ya kijeografia inakuwa vigumu kwa wakazi wa maeneo ya mbali kufikia hospitali hii.

Kuna wakati kunaagizwa Gari la wagonjwa la kumpeleka mgonjwa ambaye huwa amepelekwa kupata matibabu ya ziada kwenye hospitali kutoka kituo cha afya na ikawa vigumu kwa gari kumfikia mgonjwa kwa sababu gari huwa linalazimika kwenda safari ndefu kumfikia kwa sababu hususani ya barabara zisizo nzuri kwenye eneo hilo la vilima vilefu.

Uzabakiriho Marcel ,Raia wa Mushubati, mhudumiwa wa hospitali ya Murunda amesema “kwa kweli tumepiga hatua ya kimaendeleo lakini ningependa kuomba rais atakayechaguliwa kuijenga hospitali nyingine ya karibu. Unajua kuna wakati tunapomleta mgonjwa na analazimika kushinda usiku kwa sababu hawezi kurudi makwao na kuja hospitali kwa siku itakayofuata”.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kulingana na maelezo ya mkurugenzi wa hospitali ya Murunda inalazimika kuagiza magari ambayo ni chache kwenye vituo  vingine vinavyoweza kuwa hata mbali. “imekuwa hatari kwa magari hayo ambayo ni machache kufikisha wagonjwa, kumekuwa na wakati magari yakakwama barabarani kwa kutokana na barabara isiyo nzuri na wakati huo tukalazimika kuazima gari lingine kutoka hospitali ya Karongi ama ya Gisenyi”.

Innocent Munyakazi Makamu meya wa Rutsiro asema kuwa kuweko kwa hospitali ya pili kungerahisisha wananchi kupata huduma za afya kwa urahisi.

“tuna hospitali moja tu ambayo haifai kuwakidhi wagonjwa wa eneo hili kwa urahisi kulingana na hali ya kijeografia ya eneo hili. Ingawa tuna jinsi ya kuwahudumia wagonjwa kwa kupitia vituo vya afya na kuwasafirisha kwa magari ya wagonjwa wanaohitaji matibabu ya hospitali ingekuwa bora kukiwa na hospitali kwenye eneo la kaskazini ambayo ingewahudumia hata wakazi wa wilaya ya Ngororero kwa kuwa ingekuwa karibu.

Pendekezo la raia wa Rutsiro la kupambana na tatizo hili wakati kukisubiriwa hospitali kujengwa ni kuongeza magari ya wagonjwa kwa wingi ili kurahisisha safari zao kwenda hospitali.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.