kwamamaza 7

2017: Wasichana wa shule 17,000 wapachikwa mimba

0

Ripoti mpya ya Tume ya utawala bora kwenye seneta bungeni walitangaza kuwa wasichana wa shule za msingi na sekondari 17,000 walipachikwa mimba mwaka 2017.

Maseneta wameeleza kuwa hili ni suala la kusikitisha kulingana na waliyogundua walipokuwa ziarani ya kikazi shuleni mbalimbali  nchini Rwanda kote na kuwalaumu walimu wanavyofundisha somo la uzazi.

“Tulipofika tuliwauliza watoto wa kidato cha nne,tano na sita wenye   umri kama vile 18, 19 walikuwa hawajui mabadiliko ya mwili wao.Tulijiuliza kama hayo ndiyo waliyofundishwa”mmoja amesema

“Mimi ninajiuliza walifundishwa nini katika somo hili” ameongeza

“Wanasoma ila kuna mshangao kama mwanafunzi wa kidato cha sita ambaye alisoma haya mambo miaka iliyopita anauliza yale  suali la msingi” mwingine alisema

[xyz-ihs snippet=”google”]

“ Kunahitajika mabadiliko katika shule, inastahili kufundisha hili somo kinyume na kawaida ,siyo kupata alama tu baali kupata ujuzi utakaomsaidia baadaye maishani” amesisitiza.

Waziri makamu wa elimu Isaac Munyakazi amekubali kuwa walilegeza kuhusu hili jambo ila wanataraji kufundisha walimu na wasaidizi wa wanafunzi wa kike (matron).

“Tumeanzisha mfumo mpya wa kufundisha kwa jina ‘competence based curriculum’ ambao ni tofauti na ule wa kawaida pamoja na kuwa hamasisha walimu kubadili fikra zao husika na kufundisha somo la uzazi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Maseneta wameeleza kuwa mkakati huu hautoshi wala jambo murua ni walimu kubadili namna wanavyofundisha somo hili.

Pamoja na hili,wasichana wa shule 17500 walipachikwa mimba mwaka 2016 kulingana na utafiti wa Wizara ya Usawa wa Jinsia na Maendeleo ya kifamilia.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.