kwamamaza 7

Zambia: Serikali yaahidi kuwapa Wanyarwanda uraia

0

Serikali ya Zambia imetangaza kuwapa Wanyarwanda 4,000 uraia miaka mitatu ijayo.

Afisa kwa wajibu wa wakimbizi nchini humo, Abdon Mawere ametangazia BBC kuwa waliamua hili waliona hawa wakimbizi wanastahili kuwa  na haki za kumiliki mali waliyonayo.

“Tumeisha wapatia Wanyarwanda 1468 hati za mpito za kuhama na tunataraji kuwapatia wengine 4000. Hili litawasaidia kuishi kulingana na sheria” Mawere amesema

“Tunalenga kuwapa uraia ili watoe mchango wao katika mambo ya uchumi,maisha yao ya kesho.Walimaliza miaka mitatu bila hali ya ukimbizi” Ameongeza

Huyu kiongozi amesisitiza hili ni jambo ambalo lilikuwa likikera wakimbizi kutokana na kukosa vitambulisho.

Hili ni baada ya serikali ya Rwanda kuondoa hali ya ukimbizi tarehe 31 Januari 2017

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.