BURURUDANI

Zambia: Nyumba ya mchezaji aliyeshindwa kufunga mabao yashambuliwa

Polisi nchini Zambia wamewakamata mashabiki watano kwa madai kuwa walivamia nyumba ya mwanasoka wa timu ya taifa ya kandanda Alex N’gonga.

Mashabiki hao walishikwa na hasira kuwa Alex Ng’onga alikosa nafasi wazi za kufunga wakati wa mechi muhimu ya kufuzu kwa kombe la dunia ambapo Nigeria iliishinda Zambia bao 1-0

Mashabiki walitoa hasira zao kwa kuvamia nyumba yake iliyo mji wa Kitwe ambao waliitupia mawe, kwa mujibu wa kamishina wa polisi Charity Katanga.

“Tumekamata watu watano kwa makosa ya kuharibu mali na sasa wanazuiliwa na polisi.”

Taarifa za BBC,zina sema kwamba kushindwa kwa Zambia kuliipokonya fursa ya kufuzu kwa kombe la dunia nchini Urusi ambapo Nigeria walifuzu.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top