kwamamaza 7

Wizara ya Afya yawaonya Wanyarwanda kuhusu Ebola

0

Wizara ya Afya nchini Rwanda (MINISANTE) imewaonya wananchi kuhusu kujikinga na kuanzisha mikakati dhidi ya maradhi ya Ebola.

Wito huu ni baada ya mgonjwa wa Ebola kupatikana Wilayani Kasese nchini Uganda.

Tangazo lake la jana, limeeleza Wanyarwanda wanapaswa kujali uasafi na kuripoti wanapona dalili ya ugonjwa wa Ebola kama vile kuugua joto mwilini, kutapika, na nyingine.

Pamoja na hayo, serikali imedai kuna mikakati murua ya kukabiliana na ugonjwa huu kwa kuwalinda wananchi.

Miezi kumi iliyopita, Ebola iliwaua  maelfu ya watu nchini DRC hususani Mkoa wa Ituri na Kivu Kaskazini.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.