kwamamaza 7

Waziri Mkuu aongoza hafla ya Kiapo cha waendesha mashtaka wawili

0

Waziri mkuu wa Rwanda, MUREKEZI Anastase ameendesha kiapo cha waendesha mashtaka wawili jana tarehe 10 Juni ambao waliteuliwa na kikao cha mawaziri mwezi Mei.

Kwa mjibu wa habari hii ya Gazeti la New Times, waziri mkuu Murekezi Anastase amesema katika hafla hiyo kwamba kazi ya Uendeshaji mashtaka ni kazi ambayo inaambatana na kuheshimu Haki za Kibinadamu, uadilifu na hata kutenda haki kwa zoezi la utoaji haki sawa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Waziri mkuu Murekezi aliendelea kuwahimiza kutumia teknolojia katika utendaji kazi yao na kutoa huduma nzuri zinazohusiana na kazi yao.

“Mkumbuke ya kwamba katika sekta hii kuna waendeshaji mashtaka ambao kawaida wanatumika kazi. Na kwa kuwa serikali inasifu utumikaji kazi kwa bidii, mnahimizwa kushirikiana” asema

Aliwahimiza pia kuipanua kazi yao hadi nje ya mipaka na kushirikiana na ngazi za nje ya Rwanda na hata wa eneo la maziwa makuu kuhakikisha kwamba wahalifu wa mauaji ya kimbari wanakamatwa na kuletewa mbele ya sheria

Licha ya hayo waziri mkuu pia amebainisha uhalifu ambao waendesha mashtaka hao wataufuatialia kwa umakini ambao ni pamoja na mauaji,unyanyasaji wa nyumbani,utoaji rushwa, kuficha mali ya uma, uhalifu wa kuvuka mipaka, uuzaji wa binadamu, ugaidi na mengineyo.

Waendesha mashtaka waliokula kiapo ni Didier Rudahusha wa mahakama kuu ndogo na Claudine Kayitesi wa mahakama ndogo ambao watafanya kazi yao mjini Kigali.

Awali Didier Rudahusha amekuwa akitumika kama muendesha mashtaka wa mahakama ndogo na Claudine Kayitesi ambaye alikuwa kaimu mwendesha mashtaka.

Waendesha mashtaka wote wawili walisema baada ya viapo viapo vyao kwamba watazingatia maslahi ya umma katika utendaji kazi yao ya kila siku.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.