HABARI MPYA

Waziri Kaboneka awataka wazazi kutoingilia mambo ya uchumba wa wana wao

Waziri wa utawala wa nchi,Francis Kaboneka kwenye siku ya kuweka nje matokeo ya utafiti uliofanywa na wizara ya utamaduni na michezo kuhusu yanayonyesha ndoa kwa utamaduni wa Rwanda, amewataka wazazi kutoingilia mambo husika na uchumba wa wana wao hasa kuchagua atakaye kuwa mwanamke ama mwanamume.

Waziri Kaboneka amewakumbusha wazazi kuwa upendo una thamani zaidi ya mambo yote yenye uhusiano na kufunga ndoa.

Pia waziri huyu amesema kuwa wajibu wa wazazi ni kushauri wana wao kinyume na kuweka mahari ya hali ya juu na kuwakataza mabinti wao kuolewa na wavulana wenye ufukara.

Waziri wa maendeleo ya familia,Esperance Nyirasafari amewakumbusha wazazi kwamba mahari siyo amri ama bei lakini ni kumbukumbu na kuhamasisha jamii kubadili mwenendo huu.

Waziri  wa utamaduni na michezo,Julienne Uwacu ameleza kuwa wazazi hawana budi kufuatilia utamaduni.

Baadhi ya masuala yaliyozuka ni kuwa athari ya vitendo vya uingiliaji wa wazazi katika uchumba wa wana wao husababisha ufukara,ugomvi na talaka.

Haya yametangazwa wakati ambapo wengi mwa wazazi wananung’unika kuhusu mahari na mahitaji ya kifahari ya ndoa za siku hizi.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top