HABARI MPYA

Wawili mwa waliokuwa viongozi wa MRND watumwa kufungwa nchini Senegal

Wawili mwa waliokuwa viongozi wa chama tawala MRND mnamo mwaka 1994 wakiwemo aliyekuwa waziri wa utawala,Eduard Karemera na Mathew Ngirumpatse aliyekuwa kiongozi wa MRND wakati wa mauaji ya kimbali wametumwa kufungwa nchini Senegal.

Taarifa hizi zimehakikishwa na mahakama ya TPIR kupitia mazungumzo na Jeune Afrique kuwa watu wanne walitumwa nchini Senegal mwanzoni mwa mwezi Disemba 2017.

Wengine watakawofungwa kwenye gereza ya Sebikotane ni aliyekuwa diwani wa Muganza,kusini mwa Rwanda,Elie Ndayambaje na Arsene Sharom Ntahobali,bin Nyiramasuhuko ambaye alikuwa waziri wa maendeleo ya wanawake.

Ngirumpatse na Karemera walihukumiwa kufungwa maisha jela mwaka 2011, Shalom na Elie walihukumiwa kufungwa miaka 47.

Senegali ni nchi ya tatu kuwakaribisha wafungwa kutoka TPIR baada ya Benini na Mali.

Hili ni kufuatilia mkataba kati ya Umoja wa Mataifa kati na Senegal wa mwaka 2010.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top