Connect with us

HABARI MPYA

Watu wazima wangali na itikadi ya mauaji ya kimbali-Dk.Bizimana

Published

on

Katibu mtendaji wa Tume ya nchi ya kupambana na mauaji ya kimbali(CNLG),Dk.Jean Damascene Bizimana ameleza kuwa watu wazima wanagali na itikadi ya mauaji ya kimbali jambo  ambalo ni kikwazo kikubwa kwa jitihada za kupambana na mauaji ya kimbali.

Dk.Biziamana amesema kuwa baadhi ya wazazi hufundisha watoto wao mambo ya kikabila na kuwa kuwa haitakuwa rahisi kwa kizazi kipya kujihisi kama Wanyarwanda.

‘Kuna wasiwasi za kuwa kizazi cha siku za usoni kitakuwa na itikadi ya mauaji ya kimbali”amesema Dk.Bizimana.

Pia Kiongozi huyu kwa mjibu wa taarifa za The New Times amesema kuwa kulifanywa mengi kupambana na mambo ya itikadi ya mauaji ya kimbali kama vile kufundisha historia ya Rwanda kwa kuzuia mafunzo ovyo husika na ukabila,jambo lililosababisha mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994.

Pamoja na haya, kanuni ya adhabu kwenye makala yake 135, hutaja kuwa mtu mwenye hatia ya kuwa na itikadi ya mauaji ya kimbali anafungwa jela miaka juu ya mitano hadi tisa pamoja na faini ya frw elfu 100 hadi miliyoni moja.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook n

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Maombe
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *