kwamamaza 7

Warundi elfu sita watuhumiwa uhalifu wa mauaji ya kimbali dhidi ya Watutsi nchini Rwanda

0

Serikali ya Rwanda imetangaza kuna Warundi elfu sita wanaotuhumiwa uhalifu wa mauaji ya kimbali dhidi ya Watutsi mwaka 1994.

Mwendeshamashka mkuu nchini, Jean Bosco Mutangana kwenye mazungumzo na mwenzake wa mahakama ya IRMCT,  Dr Serge Brammertz amesema nia ya kisiasa kwa Burundi ni kizuizi kwa kuwapa haki Watutsi waliouawa.

Wakati wa mauaji ya kimbali nchini Rwanda, kulikuwepo Warundi waliokuwa wakimbizi kutokana na fujo lilikuwepo kwao mwaka 1993.

“ Kuna Warundi waliojihusiha na mauaji ya kimbali. Siku nyingi zimepita, Burundi haikuonyesha nia ya kisiasa kutusaidia kutatua suala hilo.” Amesema Mutangana

Mutangana amesema Rwanda ilitoa hati za kuwakamata watuhumiwa lakini Burundi haikufanya chochote.

Amesema wanategemea msaada wa Polisi ya kimataifa kuwakamata watuhumiwa ambao amesema wanaishi karibu na mpaka wa Rwanda kwa kutoa mfano wa Mkoa wa Kayanza na pengine.

Imeripotiwa kuwa Warundi waliwaua Watutsi katika wilaya zilizopo karibu na mpaka wa Burunid zikiwemo Nyaruguru, Gisagara na Bugesera.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.