kwamamaza 7

Warundi 16 waeleza wamefukuzwa nchini Rwanda

0

Raia wa Burundi 16 wameelezea serikali yao kuwa jana  walifukuzwa nchini Rwanda.

Taarifa hizi zimehakikishwa na Mshauri katika  mambo ya mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya usalama wa ndani nchini Burundi,  Pierre Nkurikiye kwa kueleza hawa wakazi  wamefukuzwa nchini Rwanda na kukimbilia eneo la Kirundo kaskazini mwa Burundi.

Huyu waziri  amesema hawa Warundi wamefika eneo la Gasenyi,mkoa wa Kirundo wakiwemo wanaume  wazaliwa  wake.

Wengine ni wazaliwa wa wilaya Bugabira,Vumbi  na Busoni.

Waziri wa Sheria wa Burundi Aime Laurentine Kanyana wiki iliyopita aliwataka wakazi kutotafuta kazi nchini Rwanda kutokana na kuwa Rwanda “haiwataki”.

Takwimu zinaonyesha kwamba mwaka huu, Warundi 800 walifukuzwa nchini Rwanda kwa mujibu wa Rediyo Sauti ya Marekani.

Serikali ya Rwanda jumamosi imewarudisha kwao  Warundi 115 walioingia nchini kinyume na sheria.

Pia, terehe 29 Juni mwaka huu,  Rwanda iliwafukuza Warundi 200 kwa kusema wanaishi nchini kinyume na sheria.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.