kwamamaza 7

Wapinzani wa serikali ya Rwanda waanza maandalizi ya kuishambulia nchi

0

Wapinzani wa serikali ya Rwanda wameanza maandalizi ya kukusanya fedha zitakazosaidia katika vita vya kuishambulia Rwanda.

Kupitia barua yake ndefu,aliyekuwa mwendeshamashtaka mkuu kwenye serikali ya Rwanda iliyo ukimbizini, Abdallah Akishuli ambaye ni mwanachama wa FPP-Urukatsa,inaonekana waziwazi kuwa wapinzani wanatarajia kuuza dhamana(bonds) zenye bei ya Euro miliyoni 10.

Pia kunatarajiwa kuongeza fedha hizi kulingana na yatakayohitajika kwa kutekeleza kitendo hiki kama wahenga walivyoeleza baada ya uchambuzi wao.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pia,katika barua hii kuna taarifa za kuwa Wanyarwanda ndio watakaopata fursa ya kwanza kununua dhamana hizi na kuwa fedha zitakazotolewa zitatumiwa katika vitendo vya kuipindua serikali ya Rwanda.

Barua hii inaendelea kueleza kwamba Wanyarwanda watakapogoma kuhudhuria biashara hii kutaalikwa watu kutoka nchi nyingine katika biashara hii.

Taarifa hizi zinaendelea kusema kuwa haina budi kuhamasisha Wanyarwanda kutoa msaada kwa ili kuongeza uwezo wa kutekeleza wanalolidhamiria.

Pamoja na haya,mwandishi amejaribu kushawishi wanausalama wa Rwanda kujiunga nao kwa kutia hadharani zawadi mbalimbali zitakazotolewa na vyeo watakavyopatiwa,wanasiasa kwa kutoa ahadi ya kuwapatia nafasi kwenye serikali mpya,wasanii na watangazaji.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Barua hii inaeleza kwamba familia ya Assinapol Rwigara itarudishiwa mali yao pamoja na fidia sawa na bei ya nyumba yao iliyobomolewa na kuwa tajiri  Rujugiro Tribert Ayabatwa  atarudishiwa jumba lake la kifahari lililouzwa kwa mnada kwa jina ‘Union Trade Center’ maarufu kama UTC.

Me Abdallah Akishuli alijiuzulu kwenye nafasi ya mwendeshamashtaka katika serikali ya Rwanda iliyo ukimbizini mwezi Novemba 2017.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

@Bwiza.com

 

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.