kwamamaza 7

Wanyarwanda na Warundi wakamatwa wakiwa ndani ya kituo cha jeshi la DR Congo

0

Raia wa Rwanda na wa Burundi wamekamatwa wakiwa ndani ya kituo cha jeshi cha Katindo, Kivu kaskazini nchini DR Congo kinyume na sheria.

Kiongozi wa eneo la 34 FARDC, Jen. Kamanzi ameeleza hawa walikuwa na wanawake,watoto wao na kuhakikisha wamegundua bunduki 16 aina ya AK 47,risasi 328 na ‘magazine’ 39 za risasi.

“Tumeona kwamba kuna wanajeshi waliokuwa walimiliki bunduki kinyume na sheria”

Kwa mjibu wa Radiyo Okapi, Jen. Kamanzi ameongeza wamegundua pia dawa za kulevya na kuwa zimetumwa kwenye ofisi ya uchunguzi wa jeshi.

Huyu Kiongozi amesema si mala ya kwanza kuwakamatwa Wanyarwanda na Warundi wakiwa ndani ya kituo cha jeshi

“ Tunahitaji kujua walivyofika hapa. Hii si mala ya kuanza,tuliwakuta Wanyarwanda na Warundi wakiwa ndani humu siku zilizopita”

Jen. Kamanzi amewahamsisha wakazi kuwasilaina vilivyo na jeshi ili kuakamata hawa watu kwa kuwa kuna suala la ongezeko la majambazi wenye bunduki siku hizi.

Suali ni kwamba hawa Wanyarwanda na Warundi walingia namna gani katika kituo cha jeshi cha Katindo bila msaaada wa mtu yeyote wa ndani.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.