kwamamaza 7

Wananchi waomba Rwanda na DRC kutoa suluhisho  kwa suala la wanamgambo wa FDLR

0

Wakazi eneo la Kalehe nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameomba serikali yao na ya Rwanda kutoa suluhisho kwa suala la wanamgambo wa FDLR wanaowaangamiza.

Hawa, wamefanya maandamano wakiomba hizi serikali kuwarejesha kwao wanamgambo wa FDLR.

Kwa mujibu wa gazeti la Media Congo, wakazi wa maeneo wameeleza FDLR walihamia Bunyakiri kutoka Mwenga, Kivu Kaskazini wanakochimba madini.

“ Umepita mwezi hawa Wanyarwanda wameanzisha sheria zao. Wananchimba madini milimani Kalehe na kupeleka kwao. Jambo hili linawaletea wasiwasi wakazi wa Bunyakiri.” Amesema Kiongozi wa Shilika la Buuma bw’Ebatembo, Xavier Mulirima Baricirongo

“ Kupitia njia za kidiplomasia tunataka ha wa wanamgambo warudishwe kwao. Tunaomba hili litekelezwe haraka ili waondoke kwenye ardhi yetu.” Wakazi wameandikia mkoa.

Wanamgambo wa FDLR wanaishi nchini DRC tangu mwaka 1994. Wanashyakiwa uahlifu ukiwemo ubakaji,  vitendo vya kigaidi na mengine.

 

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.