kwamamaza 7

Wanahabari wapata msaada wa kufikia malengo waliyojitolea kuyafikia

0

Wanahabari walioshiriki mafunzo  ya kujifunza mila na maadili ya wanyarwanda(itorero) katika migawanyiko ya vipindi viwili ya wanahabari waliopewa jina la ‘Impamyabigwi’ wameahidiwa ufadhili wa milioni tatu (3,000,000) kama msaada wa kuyafikia malengo waliyojitolea kuyafikia.

Ufadhili huu waliopewa na Prof. SHYAKA Anastase, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Nchi (RDB) ulikuwa kwa madhumuni ya kuwasaidia kuanzisha shirika la kuwekeza na mikopo la IMPAMYABIGWI Media SACCO kwa haraka iwezekanavyo.

Kwa hivyo Mkurugenzi wa RDB Shyaka Anastase akawahimiza kuyafikia malengo waliyojitolea kuyafikia yakiwemo kuanzisha kwa haraka shirika hili. Prof. Shyaka ametangaza haya baada ya mchezo uliowakutanisha wanahabari hao waliojigawa katika makundi mawili kulingana na vipindi walivyoshiriki mafunzo hayo.

Shayaka anastase amesema kwa kuonyesha sheki  ya karatasi pana iliyokuwa ikiandikwa milioni 3 “ hii ni ishara ya kuwatia moyo wa kuanzisha shirika hili mapema iwezekanavyo ni kumaana mkianza  shirika udhamini wenu mtapata kwa mara”

[xyz-ihs snippet=”google”]

Katika mchezo huo kundi la kwanza la ‘Impamyabigwi’ liliwashinda ‘Impamyabigwi II” kwa mikwajuu ya penati na kutwaa kombe. Na hii ni baada ya dakika za kawaida kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Ni mara nyingi tatizo la Uwezo wa kifedha lililojitokeza kwa wanahabari kwa sababu ya mshahara mdogo wanaolipwa au mojawapo kutopata.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 

Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.