kwamamaza 7

Walevi barabarani kukamatwa nchini Uganda

0

RFI

Polisi nchini Uganda inapania kuzindua mpango wa kuwakamata watembea kwa miguu watakaopatikana wakiwa walevi.

Akitetea mpango huo mpya kamanda wa trafiki katika jiji la Kampala Lawrence Niwabiine amesema kikosi cha polisi hakitaruhusu watu “wahatarishe”maisha yao.

Tayari vyombo vya habari nchini Uganda vimezua gumzo mitandaoni baada ya kuangazia mpango huo tata katika mitandao ya kijamii.

Watu wamekua wakihoji jinsi sheria hiyo itakavyotekelezwa hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya watu wanaokamatwa kila uchao wakiendesha magari wakiwa walevi huishia kuachiwa katika mazingira ya kutatanisha.

Hata hivyo kuna mamia ya watu waliyopatikana na hatia ya kuendesha magari wakiwa walevi wameshindwa kulipa faini.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.