kwamamaza 7

Wakazi wa eneo la volkano wapewa mafunzo ya kujikinga wakati wa mlipuko

0

Kumetolewa masomo ya kuwasaidia watu kujikingia wakati wa kufoka kwa volkeno ambayo amejumuisha wakazi wa Rubavu ya Rwanda na majirani yao ya Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

 Katika hafla hii kumefanyika safari mjini Goma wakazi wa maeneo hayo wamepitia mahali palipoharibika kupitia mlipuko wa volkeno ya Nyiragongo wa 2002. Walionyeshwa na kuelezewa pia dalili za mliipuko wa volkeno ikiwemo tetemeko la ardhi, na hata rangi zilizochorwa na Idara ya Utafiti kuhusu milipuko wa Volkeno (OVG).

Hata hivyo wakazi hao walionyesha mashaka kwamba huenda wanakemewao kwamba kuna mlipuko wa unaokaribia kujitokeza.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwa kuondoa mashaka hayo, Bwiza.com ilimhoji Mwenyekiti wa Shirika la Msalaba Mwekundu na hata masuala ya milipuko wa volkeno. Alihakikisha kwamba haina uhusiano wowote.

“volkeno ziko mpaka sasa katika rangi ya manjano na rangi hiyo haionyeshi dalili za kulipuka ila nyekundu ndio mbaya. Tumeamua kuwafundisha wakazi kuhusu jinsi wanavyoweza kujikinga wakati wa mlipuko wowote”

Afisa mtafiti wa idara ya Utafiti kuhusu mlipuko wa Volkeno katika eneo la Kivu Kaskazini nchi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo alieleza kwamba shughuli za kuwafundisha wakazi wa maeneo ya karibu ya Volkeno ni kawaida kwa nchi zenye hatari kama hiyi.

Aliendelea kusema kwamba mfano wa Ujapani kunafanyika shughuli kama hizi na wakazi huwa wanajua la kufanya wakati wa tukio kama hili. Huwa wanahamisha hazina na vifaa vinavyoweza kuharibika kama fedha, magari na mali nyingine na hata kuandaliwa mahali pa kuhifadhia wakimbizi.

Aliongeza kwamba ndio sababu shughuli hii ilijumwisha ngazi mbalimbali wakiwemo wakazi, madaktari na wauguzi, askari jeshi na polisi na hata watangazaji habari ili waweze kueneza habari hii na kuieleza kwa wakazi wa maeneo ya Volkeno.

Fellen lutaichibwa, Kaimu Gavana wa Jimbo la Kivu ya Kaskazini alihimiza nchi zinazopakana na volkeno hizi kuwa na ushirikiano wa pamoja kwa kupambana na madhara yanayoweza kusababishwa na milipuko ya volkeno. Hapa alidokeza kwamba mlipuko haubainishi mpaka.

Shughuli za kuwafundisha wakazi wa maeneo ya Volkeno kuhusu jinsi ya kujikinga zitaendelea kwenye wilaya ya Rubavu na zitafanyiwa pia nchini Uganda kwa raia wakazi wa maeneo ya karibu na volkeno ya nchi hiyo.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Richard Wa Billy

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.