kwamamaza 7

Vijana wa shirika la CEEVA wafurahia kiwango cha maendeleo nchini Rwanda

0

Vijana 80 kutoka nchi 35 baada ya kufika  nchini Rwanda kuiga mengi hasa namna ya kulinda amani,usalama,umoja na maridhiano wameshukuru kiwango cha maendeleo nchini  Rwanda.

Vijana wa Shilka la CEEVA waliokuja kuiga mengi kwa nchi ya Rwanda

Kama ilivyotangazwa na katibu mtendaji wa CEEVA (Communaute Evangelique d’Action Appostlique) duniani,Rev.Pastor Emmanuel Desire Johnson vijana hawa watua Rwanda baada ya kutoka nchi nyingine tofauti  wakati wa wiki mbili.Ameeleza kuwa wamekuja Rwanda kwa kuwa ina mifano kadhaa ya kuiga  inayoweza kusaidia vijana hawa kwa mapana na marefu.Rev.Pastor Emmanuel Desire amesema ”Tulikuwa na uzowevu wa kuenda ulaya lakini tuliona kuwa Rwanda ina mengi ya kutufundisha kuliko kwingine”.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pengine kiongozi wa CEEVA nchini Rwanda,Munyankindi Epimaque ameshukuru shirika hili kwa kuchagua kuja kuiga Rwanda kwa kuwa ni furaha kubwa kwa kueleza”Tumefurahi sana kwa kutuchagua barani Afrika”.Vijana hawa wamepata fursa ya kuwashauri wenzao kutojihusisha na utendaji maovu na vitendo vya kigaidi na mengine.

Hili lasisitizwa na katibu mtendaji wa mkoa wa magharibi,Habiyaremye Pierre Celestin ambaye amewomba vijana hawa kuwa wazalendo na kuiga mifano ya viongozi wazuri wa bara la Afrika na kutoa michango yao kwa maendeleo ya shirika la ‘panafrican’ na kuwashukuru kwa kuja kuiga nchi ya Rwanda.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.