kwamamaza 7

Ushirikiano na vyombo vya habari unatufanya kufikia uhuru wa maoni- Busingye

0

Waziri wa sheria na ambaye ndiye mwanashria mkuu wa serikali ya Rwanda ameongoza mazungumzo kati ya waandishi wa habari ambapo amesema ushirikiano kati ya wanahabari na Polisi na idara zenye madaraka ya kutunza na kutetea sheria ndio unaotufanya kupiga hatua mbele.

Waziri Busingye amesema hayo akiwa katika mazungumzo na waandishi wa habari na ngazi nyingine zenye madaraka ya kutunga sheria, mazungumzo ambayo yamekamilishwa tarehe 11 Julai kwenye makao makuu ya Jeshi la Polisi ya Rwanda(RNP)

Katika mazungumzo haya walikuwemo viongozi wakuu wengine kama Mkuu wa Jeshi la Polisi ya Rwanda IGP GASANA K.Emmanuel, Kaimu wake wa Utendaji DIGP Dan Munyuza na hata Charles Munyaneza, Katibu Mtendaji wa Tume ya Uchaguzi ya Rwanda,Mkuu wa taasisi ya wandishi wa habari huru, Afisa kutoka RURA, Afisa kutoka wizara ya mambo ya ndani ya nchi na hata wanahabari mbalimbali.

Katika hotuba yake ,Busingye Jonhston Mwanasheria Mkuu wa Rwanda ametangaza kwamba wakati huu Vyombo vya habari vimesonga mbele kuliko wakati wowote wa Historia na ni ishara kwamba kesho patakuwa pazuri “wakati huu na kesho ni wakati wenye uhuru, wakati wa haki ya maoni na hiyo inata imani kwamba kesho patakuwa pazuri kuliko wakati wowote wa historia”

Mazungumzo haya ambayo yaliendeshwa katika Jimbo nne za nchi juu ya mada “ Endeleeni ushirikiano kwa lengo la kutoa huduma nzuri” na hii ina madhumuni ya kuimarisha ushurikiano kati ya vyombo vya habari na ngazi nyingine za serikali huku kukizingatiwa maslahi ya jamii.

Waziri Busingye aliendelea kusema kwamba ushirikiano kati ya vyombo vya habari na polisi na hata ngazi nyingine zenye madaraka ya kutunza na kutunga sheria ndio unaotufanya kufikia  uhuru ambao unazingatia lenye faida kwa wanyarwanda. “ Mnapaswa kuzitangaza habari zenye maudhui muhimu kwa wanyarwanda zisizo na ubaguzi ambayo yalikuwa pigo kwetu na habari ambazo zitakuwa muhimu katika maisha  ya Munyarwanda ya kila siku.

Alisema kuhusu uchaguzi kwamba kunahitajika ushirikiano ili kuuendesha salama uchaguzi kwa kuwa ni uturatibu usio wa kudumu na baadaye maisha huenda kama kawaida.

Kiongozi mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Gasana Emmanuel naye alichukuwa muda wake kuwashkuru waandishi wa habari kwa kuwa wanachangia kupambana na uhalifu.

Aliongeza kwamba Polisi itakuwa tayari kulinda usalama wa mahali pote ambapo uchaguzi utaendeshwa kwenye vituo vya uchaguzi ambavyo vimeenezwa nchini mwote.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Na kuhusu usalama wa barabara IGP Gasana alisema kwamba Polisi iliileta mashine ya kupima magari yasiyokidhi vigezo vya ubora na ambayo yangeweza kusababisha kutokea kwa ajali na mashine hii itatumiwa wakati wa uchaguzi.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Uchaguzi Bw Charles Munyaneza yeye aligusia kuhusu haki ya kupata habari ambapo alisema waandishi wa habari wana haki ya kupata habari wakati huu wa Uchaguzi kwa kuwa wana wajibu wa kuwatangazia wanyarwanda yanayoendelea nchini mwao.

La hasha, amewaonya kuwa hawana haki ya kutangaza Motokeo ya kura kabla ya tume ya Uchaguzi kufanya hivyo

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.