kwamamaza 7

Ujerumani yatwaa ubingwa wa mabara

0

Baada ya ureno kushinda nafasi ya tatu katika mashindano ya Kombe la mabara ujerumani nao watwaa ubingwa wakiilaza Chile kwa 1-0. Kupitia goli lililopatikana mapema dakika ya 20 ya mchezo.

Mshindi wa goli la Ujerumani alikuwa Lars Stindi. Ujerumani yashinda Ubingwa huu kwa mara ya kwanza na inazidi kuonyesha nguvu na matumaini ya kufanya mengi wakati kesho wakiwa ndio mabingwa wa Kombe la Dunia na kikosi chao cha sasa kikiwa kina wachezaji wa umri mdogo.

Katika mechi hiyo vile Chile walionyesha nguvu za hali ya juu wakitaka kusawazisha ila matumaini yao hayakuwezekana hadi dakika ya mwisho.

Na hatimaye Ureno ilifanikiwa kuishinda Mexico kwa bao 2-1, katika mchezo ambao walicheza bila kuwepo kwa nyota wao Cristiano Ronaldo aliyeiacha timu yake na kujiunga na familia yake baada ya kutangaza kwamba yeye kwa sasa ni baba wa mapacha.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Luis Neto, Beki wa Ureno ndiye aliyewapa Mexico bao la kuongoza baada ya kujifunga mwenyewe dakika ya 55 ya mchezo. Isitoshe Ureno ingawa iliucheza mchezo huyu licha ya kutoweko kwa nyota wao Ronaldo ilionyesha shauku kubwa kwa kushinikiza timu ya wapinzani wao Mexico hadi Pepe kusawazisha katika dakika za Mwisho wa mchezo na kuwalazimisha kucheza dakika 30 za nyongeza.

Dakika ya 104 ndiyo ilikuwa maumzi ya mechi hiyo wakati Adrian Silva alipoipatia timu yake ya Ureno bao la pili kwa mkwajuu wa penati .

Chile walifika fainali baada ya kuwachapa Ureno katika nusu fainali kwa mikwajuu ya Penati ambapo Kipa wake Claudio Bravo alionyesha uhodari mhimu wa kuokoa timu yake kwa kutoingizwa hata penati moja mwa tatu alizopigwa.

Ujerumani nayo ilifuzu kucheza fainali baada ya kuangamiza Mexico kwa ushindi mnono wa mabao mane kwa moja na hivyo basi wakaongeza matumaini yao ya kushinda kombe hili kwa mara ya kwanza ya historia yake.

Michezo hii inafanyika mwaka mmoja kabla ya Kombe la Dunia kuchezwa ambapo la mwaka jana litafanyika kuanzia mwezi wa Juni wa mwaka wa 2018 hapo Urusi.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.