HABARI MPYA

Uganda:Wanasheria wa Wanyarwanda 45 waliokamatwa watoa ombi mahakamani

Wanasheria wa Wanyarwanda 45 waliokamatwa,KOB Advocates wamefika mahakamani wakilalamikia kuendelea kufunga wateja wao kwenye kituo cha polisi cha Nalufenya tangu walipokamatwa tarehe 11 Disemba 2017.

Wanasheria wametangaza kuwa Wanyarwanda hawa wameshikiliwa juu ya masaa 48 na kuwa hawakufika mahakamani husika na wanayoshtakiwa ili kuhukumiwa,mambo ambayo ni kunyume na sheria.

Taarifa za Chimpreports zinaeleza kuwa Wanasheria wameongeza kwamba serikali iliwakataza ama kushindwa kuwawezesha kuwasiliana na wateja wao.

Pia walimuandikia kiongozi wa polisi ya nchi,Jenerali Kale kayihura terehe 18 Disemba ili kuwapatia idhini ya kuwasiliana na wateja wao lakini haikuza matunda.

Pengine kuna barua nyingine ya terehe 21 Disemba 2017 ambayo wanasheria waliandikia ukurugenzi wa mashtaka ya umma,DPP wakilalamikia jambo hili.

Wanyarwanda hawa ni wakimbizi kutoka kambi ya Nakivale,walikamatwa wakijaribu kuvuka mpaka kati ya Tanzania na Uganda,Kikagati wakienda kwa shughuli za kidini nchini Tanzania.Hata hivyo, kuna taarifa kwamba walikuwa wakielekea nchini DR Congo kujiunga na  jeshi la RNC na nyingine za kuwa wana uhusiano na waasi wa ADF.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top