HABARI MPYA

Uganda:Mnyarwanda mwingine akamatwa na upelelezi

Mnyarwanda mwingine kwa jina la Fidele Gatsinzi amekamatwa na mafisa wa upelelezi wa Uganda kwa kutuhumiwa kuwa mpelelezi wa Rwanda.

Taarifa hizi zimehakikishwa na ubalozi wa Rwanda nchini Uganda kupitia mshauri wake wa kwanza,Noel Mucyo akizungumza na Chimpreports.

Mwanasiasa huyu amesema kuwa Fidele Gatsinzi alikamatwa na mafisa wa upelelezi wa Uganda (CMI) Tarehe 9 Disemba 2017 na kuwa hana lolote la kunena kuhusu kisa hiki kwa kuwa suala hili halikuwasilishwa kwenye ubalozi wa Rwanda.

Pia huyu ameongeza kuwa wanalolijua ni kwamba Gatsinzi hana hatia.

Hili ni baada ya taarifa za kuwa Wanyarwanda karibu elfu moja walifungwa kwenye jela mbalimbali nchini Uganda wakituhumiwa kuwa wapelelezi wa Rwanda.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top