Connect with us

HABARI MPYA

Uganda:Mkazi asili ya Rwanda atoweka baada ya kutekwa nyara

Published

on

Mkazi wa wilaya ya Ntungamo asili ya Rwanda,Johnson Nuunu ametoweka  baada ya kutekwa nyara jumanne usiku akiwa baani .

Taarifa hizi zimejulikana kupitia nduguye Eric Kinote katika mazungumzo na NTV,nchini Uganda alipoeleza kuwa Johnson Nuunu ametoweka baada ya kutekwa nyara na watu wanaotuhumiwa kuwa wanausalama na kuwa  walijulisha suala hili kwenye kituo cha polisi ila hawakusaidiwa lolote.

Pia mpwa wake,Amon Tumusiime amabaye walikuwa pamoja baani, ametangaza kuwa watu wasiojulikana walikuja na kumuweka garini Johnson na kuondoka kwa kasi na kuwa yeye hakuweza kuwajua.

Bin Johnson Nuunu,Joseph Kanyesigye ameleza kuwa baaba yake hana uhusiano wowote na siasa,jeshiama polisi na kwa hiyo hawajui chanzo cha kisa hiki.

Haya ni baada ya Wanyarwanda karibu elfu kukamatwa na kufungwa nchini Uganda kwa kutuhumiwa kuwa wapelelezi wa Rwanda,jambo ambalo kupitia ubalozi wake nchini Uganda serikali ya Rwanda iliomba maelezo zaidi ya vitendo vya kuwakamata Wanyarwanda.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Maombe
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *