kwamamaza 7

Uganda:Mafisa wa upelelezi ‘waunga mkono’wanachama wa RNC kuwakamata Wanyarwanda

0

Mnyarwanda Fidele Gatsinzi aliyekamatwa na mafisa wa upelelezi  nchini Uganda(CMI) ametangaza kwamba kuna ushirikiano kati ya CMI na wanachama wa RNC katika mambo ya kuwakamata Wanyarwanda kwa kuwashtaki kuwa wapelelezi wa Rwanda.

Fidele Gatsinzi baada ya kuteswa kimwili wiki nzima na kuachiwa huru kwa kutupwa kwenye mpaka kati ya Rwanda na Uganda ametangazia The Newtimes kuwa mafisa wa CMI wanasaidiana na wanachama wa RNC hasa Rugema Kayumba na mwingine Mukombozi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pia amesema kuwa Rugema Kayumba na mwenzake ndio waliomuweka garini kwa nguvu na kumpeleka katika nyumba ya siri eneo la Ntinda,mjini Kampala.

Hili ni baada ya mafisa wa upelelezi nchini Uganda hasa kiongozi wa CMI Brig.Gen.Abel Kandiho hasa waziri wa usalama Jenerali Henry Tumukunde kuhusishwa na suala la wakimbizi asili ya Rwanda na kushirikiana kidhati na kiongozi wa RNC Jenerali Kayumba Faustin Nyamwasa

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.