HABARI MPYA

Uganda:Mafisa wa ISO washtakiwa kuwateka nyara wakimbizi asili ya Rwanda ili kujitajirisha

Mafisa wa ofisi kuu ya usalama wa ndani nchini Uganda (ISO) wanashtakiwa kuwateka nyara na kuwababaisha  wakimbizi asili nchini Rwanda kwa kuwaomba fedha  ili wasirudishwe nchini kwao.

Taarifa hizi zimesamabaratika baada ya mikimbizi asili ya Rwanda,Jean Paul Cyubahiro aliyetekwa nyara tarehe 27 Octoba mwaka 2017 alipokuwa kwenye barabara la Nasser anapofanyia kazi kama Graphics Designer.

Taarifa za Spyreports zinasema kuwa huyu alipofika gerezani,mafisa wa ISO walimpigia simu mwanafamilia wake,Innocent Nyandembwe wakimuomba kutuma shilingi 500,000 ili kumuachia huru Cyubahiro.Nyandembwe alituma fedha hizi lakini mafisa hawakumuachia huru Cyubahiro.

Baada ya hili, Cyubahiro alifungiwa mjini Kampala alipolindwa na afisa wa ISO kwa jina la Franco amabaye alimshawishi namna ambavyo anaweza kumlipa shilingi miliyoni moja kwa kumsaidia kutoroka.

Cyubahiro  alikubali ushauri huu wa kumpa fedha,Innocent Nyandembwe aliwaita polisi alipokuja kumpa Franco fedha hizi  kisha Franco akakamatwa hapohapo akipokea fedha eneo la City Square mjini Kampala.

Pamoja na haya kuna taarifa za kutoelewana vizuri kati ya mafisa wa ISO na mafisa wa Ofisi ya upelelezi wa kijeshi,CMI,mkurugenzi wa CMI,Kanuni Abel Kandiho aliishtaki ISO kuwakamata watu bila hatia na kuwafungia katika magrereza ya CMI.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top