HABARI MPYA

Uganda:Afisa mkuu wa polisi ashtakiwa kumteka nyara Mnyarwanda

Afisa wa polisi SSP Nixon Agasirwe, 47 ambaye angali jelani juu ya mashtaka ya uteka nyara, ameshtakiwa tena kumteka nyara Mnyarwanda mwingine Vincent Kalisa,kijijini Bukooli,wilaya ya Luweero.

Kwa mujibu wa taarifa za Chimpreports mwendeshamashtaka amedai kuwa SSP Nixon Agasirwe na mwenzake Semujju Abdulnur maarufu kama Minana walimteka nyara Vincent Kalisa tarehe 13 Ogasti 2017, kitendo ambacho ni kinyume na kanuni za kuadhibu,makala yake 239 nchini Uganda.

Taarifa hizi zinaendelea kusema kwamba suala hili limezusha kutoelewana kati ya kiongozi wa mahakama ya kijeshi Makindye,Luteni Jenerali Andrew Gutti na mwanasheria wa watuhumiwa,Frank Kanduho ambaye amekanusha mashtaka haya mapya kwa mteja wake.

SSP Agasirwe mekanusha mashtaka ya kumteka nyara Kalisa na mwenzake Minana hakunena lolote kwa kuwa hana mwanasheria.

Pamoja na haya, SSP Nixon Agasirwe pamoja na wenzake nane walikamatwa kwa kutuhumiwa kumteka nyara aliyekuwa mlinzi wa Rais Kagame.Luteni Joel Mutabazi na mwingine kwa jina la Jackson Karemera.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top