BURURUDANI

Uganda yaonyesha dalili za kufuzu kombe la dunia mwaka 2018

Timu ya Taifa ya Uganda inaendelea kuwonyesha kwamba ina uwezo wa kufuzu kombe la dunia mwaka 2018.

Emmanuel Okwi akishangilia baada ya kufunga goli

Ni baada ya kuichapa Misri goli 1-0, jambo lililongeza bahati zake kufuzu kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Goli hilo la kipekee limepatikana kupitia kwa mshambuliaji wa klabu ya Simba, Emmanuel Okwi kunako dakika ya 52 ya kipindi cha kwanza.

Kwenye msimamo wa kundi E kwa sasa Uganda wanaongoza kwa pointi 7 wakifuatiwa na Misri pointi 6, Ghana pointi 1 na Congo wakishika mkia kwa alama 0.

Mchezo huo ambao ulikuwa wenye ushindani zaidi kutokana na timu hizo kupigana vikumbo kwenye nafasi ya kwanza na ya pili kwenye msimamo wa kundi E linaloundwa na timu za taifa za Ghana na Congo Brazaville.

Mechi za kufuzu kombe la dunia 2018 zitaendelea ambapo Nigeria watavaana na Cameron, Tunisia vs DR Congo, Morocco vs Mali, Cape Verde vs Afrika Kusini na Ghana watavaana na Congo.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top