kwamamaza 7

Uganda yakamata na kuwarudisha kwao Wanyarwanda 72

0

Serikali ya Uganda jumatatu wiki hii iliwarudisha kwao Wanyarwanda 72 juu ya kuingia nchini bila vitambulisho.

Hawa Wanyarwanda wakiwemo  watoto 11, wanawake 20 na wanaume 41 wamekamatwa eneo la Rukiga na kurudishwa kwao kupitia mpaka kati ya Rwanda na Uganda kwa jina la Katuna.

Kiongozi wa Rukiga, Emmy Ngabirano ameeleza, kama ilivyotangazwa na Dailymonitor, hawa hawakuwa na vitambulisho vya kusafili nchini na kuwa hili ni kinyume na sheria.

Wengi mwa waliorudishwa nchini Rwanda  wameeleza walikua wanataka kuelekea kufanya kazi za  kawaida magharibi mwa Uganda.

Ngabirano amewaonya  madereva wanaosafili nchini Uganda  hawana budi kuchunguza kama wateja wao wana vitambulisho vyote.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.