kwamamaza 7

Uganda: Wanafunzi kutoka Rwanda waishi kwa hofu

0

Wanafunzi  kutoka Rwanda wanaosema nchini Uganda wamedai kuishi na hofu juu ya kuchungwa kila popote kwa tuhuma za kuwa wapelelezi wa Rwanda.

Wametangaza wenzao hawawamini na kuwa maafisa wa usalama wanawachunga mno. Mmoja wao wa kike, 23, amesema wananyimwa huduma na wanambiwa kurudi kwao mala nyingi.

Mwenzake anayesomea Chuo Kikuu cha Makerere amesema hali hii imekuwa kawaida na inakuwa mbaya zaidi wanapakamata Mnyarwanda akiwa na kosa.

“ Tunakwenda kwa unyenyekevu kama wanaobeba mayai, wanafikiri sisi ni wajasusi. Ukiwa na kosa, kwao ni fursa ya kuuliza unayoyajua hata na yale ambayo hujui.”amesema

Wameambia vyombo vya habari nchini humo kwamba wanakaribia mwisho wa mhula, lakini, wamesema, haitakuwa rahisi kurudi nchini Uganda kusoma kurokana na ushirikiano ovyo kati ya hizi nchi.

Ushirikiano ovyo kati ya Rwanda na Uganda ulianza miaka miwili iliyopita juu ya masuala ya kidiplomasia. Hili liliathiri mno biashara, ushirikiano na mambo mengine kwa kila upande.

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.