kwamamaza 7

Uganda: Ulinzi mkali waonekana wakati ambapo Mnyarwanda anayeshtakiwa kumteka nyara mlinzi wa Rais Kagame asimama kizimbani

0

Ulinzi mkali umeonekana leo kwenye mahakama ya kijeshi Makindye,mjini Kampala anaposhtakiwa Mnyarwanda Rene Rutagungira kumteka nyara aliyekuwa mlinzi wa Rais Kagame,Luteni Joel Mutabazi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Taarifa za Chimpreports zinasema kuwa watu tisa wakiwemo mafisa watano wa cheo cha juu wa polisi ya Uganda wanashtakiwa kumteka nyara raia wan chi nyingine kinyume na sheria ya kuadhibu,makala yake 242.

Muendesha mashtaka anawashtaki watuhumiwa kumiliki bunduki na grunedi tarehe 25 Octaoba 2017 eneo la Mpigi kinyume na sheria.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Washtakiwa walikanusha mashtaka yote kupitia wanasheria wao Evans Ochieng na Caleb Alaka tarehe 27 Octoba 2017.

Aliyekuwa mlinzi wa Kagame,Luteni Joel Mutabazi alihukumiwa kufungwa maisha jela.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pamoja na haya,serikali ya Rwanda  kupitia msemaji wa polisi,ACP Theos Badege siku zilizopita  ilikosoa kitendo cha kumshtaki  Rene Rutagungira kwa kusema kuwa kukamatwa kwake kulifuatilia sheria za kimataifa kwa kuwa jina lake lilionekana kwenye orodha ya wakimbizi wanaowindwa na polisi ya kimataifa,Interpol.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.