Connect with us

HABARI MPYA

Uganda na DR Congo:Kiota cha watuhumiwa wa mauaji ya kimbali

Published

on

Nchi ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zinatajwa kuwa makazi ya watuhumiwa wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994 nchini Rwanda.

Taarifa za KT Press zinasema kwamba 55% za watu 835 wanaishi nchini DR Congo  na Uganda baadhi ya nchi 34 dunia nzima.

Uendeshamashtaka wa Rwanda umetangaza kwamba karibu 254 wanaishini nchini DR Congo na 226 wanaishi nchini Uganda.

Afisa  kwa wajibu wa ufuatiliaji wa wahalifu wa mauaji ya kimbali,Jean Bosco Siboyintore ameeleza kuwa wanaoishi nchini jirani ni wale ambao hawakueza kukimbilia nchini za mbali na kuwa wengi mwao ni wanajeshi.

Huyu ameongeza kuwa kuna wasiwasi kutokana na kuwa nchi hizi zenye watuhumiwa wa mauaji ya kimbali  hazina  juhudi za kufanya lolote la kusaidia Rwanda hata kama hati za kukamatwa zilitumwa mwaka 2007.

Nchi nyingine yenye watuhumiwa wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994 ni Ufaransa(42),Malawi(42),Ubelgiji(39) na Kenya(28).

Bw Jean Bosco Siboyintore amehamasisha nchi hizi kutoa mchango wake kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Maombe
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *