kwamamaza 7

Uganda: Jen. Kale Kayihura ni mgonjwa mahututi alipofungiwa

0

Maisaha ya Jen. Kale Kayihura yangali hali mbaya alipofungiwa Makindye,  mjini Kampala.

Kwa Mujibu wa Spyreports, Kayihura kwa ghafla wiki iliyopita alianza kutapika na kuvimba mwili mzima karibu kufariki chumbani mwake.

Mmoja ametangazia hiki chombo “Jumamosi usiku, Jen Kayihura alianza kutapika na mwili wake ukaanza kuvimba”

Huyu ameongeza Kayihura ameshindwa kula kwa kusema hayuko katika hali nzuri.

Walinzi wa huko Makindye waliwapigia simu wakubwa wako na kuwajulisha kuhusu hili jambo la Kayiura kuomba kuenda kufanyiwa uchunguzi kwenye hospitali ya Case, mjini Kampala.

Hata hivyo, viongozi wamepiga marufuku hili ombi kwa kusema atatibiwa ndayi ya kituo cha jeshi Makindye.

“Kama  Jen Kayihura ni mgonjwa, tunaweza kuwaita madaktari gwiji kutoka Bombo na kumtibu huko Makindye. Hatuwezi kumruhusu kuenda nje” Jen. mmoja maesikikia akisema

Kwa hili,hizi taarifa  ni kwamba kufika Jumatatu Kayihura amekataa kutibiwa na madakatari wa jeshi la Uganda UPDF.

“Kayihura hajaamua la mwisho kuhusu kutibiwa na madaktari wa UPDF”

Pamoja na hayo,Msemaji wa UPDF  Brig.Richard Karemire jumatano alikanusha taarifa kwamba Kayihura ni mgonjwa

“ Hakuna taarifa kam hizo kuwa Kayihura ni mgonjwa huku Mkaindye” alisema

“Ikiwa ni mgonjwa atatibiwa huko kwani ana haki za kutibiwa” aliongeza Karemire

Jen. Kale Kayihura alikamatwa tarehe 13 Juni kwake Kashagama, wilayani  Lyantonde.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.