kwamamaza 7

Ufaransa:Mahakama yakanusha kuhukumu  waliokuwa viongozi wa wanajeshi wakati wa mauaji ya kimbali nchini Rwanda

0

Mahakama mjini Paris,Ufaransa jana imeamua kutohukumu waliokuwa viongozi wakuu wa jeshi la Ufaransa mwaka 1991-1994 yaani (Rtd)Gen.Amiral Jacques Laxande na makamu wake (Rtd) Gen.Raymond Germanos wakati wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mahakama hii imekubali uamuzi wa jaji aliyefanya upelelezi kuhusu ushiriki wa jeshi la Ufaransa katika mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi eneo la Bisesero, tarehe 27-30 Juni mwaka 1994, kusini magharibi mwa nchi wa kuwa haina maana kupeleka kesi hii mahakamani kwa kuwa hakuna ushahidi wa kutosha.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Taarifa za RFI zinasema kuwa upande mwingine wa asasi za kiraia kama Survie na FIDH wamesema kuwa kutoulizwa kwa viongozi hawa kutakuwa chanzo cha kuharibu upelelezi husika na ushiriki wa Ufaransa katika mauaji ya kimbali nchini Rwanda.

Pamoja na haya,wanajeshi wa Ufaransa waliokuwa kwenye operesheni kwa jina la ‘Operation Turquoise’ hazikuwanusuru waliokuwa wanawindwa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Serikali ya Rwanda inashtaki Ufaransa kushiriki katika mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994 kwa kusaidia  jeshi la serikali ya Juvenal Habyarimana.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.