kwamamaza 7

Ufaransa waonya wananchi wake kutembea mahali patatu nchini Rwanda

0

Wizara ya Mambo ya Nje nchini Ufaransa imewaonya raia wake kutembelea nchini Rwanda isipokuwa mahali patatu.

Tangazo lake la jana tarehe 21 Aprili lilisema Wafaransa wasikanyage katika mbuga za wanyama milimani Virunga, msituni Nyungwe hasa kutumia barabara nambari sita huko kusini magharibi kuelekea Wilyani Nyamagabe. Pengine ni na maeneo ya karibu na mpaka wa Rwanda na Uganda kutokana na kutoelewana kati ya hizi nchi mbili tangu miaka miwili iliyopita.

Tangazo linasema Wafaransa wanaotaka kwenda nchini Uganda wasitumie mbinu za barabara. Wameshauriwa kutumia njia za angani.

Hata hivyo, tangazo halikueleza kwa mapana na marefu sababu ya maonyo hayo.

Kwa upande mwingine, viongozi nchini Rwanda hasa wa usalama waliwambia wananchi kwamba kuna usalama nchini nzima.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.