HABARI

Tunakula msazo kwenye sikukuu ya Krismasi-Watoto wa mitaani

Watoto wa mitaani mjini Kigali eneo la Nyamirambo maarufu kama Nyamijisoji wametangaza kuwa wanakula msazo wa vyakula kutoka nyumba za matajiri kwenye sikukuu  ya krismasi.

Wakizungumza na VOA jana saa saba usiku, kila mmoja akiwa na chupa la kinywaji cha kulevya wametangaza kuwa wanangojea kula vyakula wanavyopatiwa kwa jina’Umusigi’ yaani msazo.

Akijibu namna ya kusherekea sikukuu,mmoja wao amesema kuwa wanafua nguo zao kisha wakatembelea kila nyumba wakiwatakia sikukuu njema kwa kuomba wali.

Pia wameongeza kuwa wanapendana sana kwa kuwa lengo lao ni kutafuta chakula.

Pamoja na haya,watoto wa mitaani wanaongezeka kila siku kufuatia matatizo yaliyomo katika familia kama vile umaskini,ugomvi na mengine.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top