HABARI

Tume ya kutetea haki za binadamu yashtaki wachuuzi ukiukaji wa haki za watoto

Tume ya kutetea haki za binadamu nchini Rwanda imewashtaki wachuuzi wadogo kukiuka haki za watoto hasa ule wa kijinsia.

Tume hii imeleza kuwa  suala hili limeongezeka kulingana na utafiti ilioufanywa mwaka 2015-2016 na kuwa ripoti yake ya mwaka huu inayonyesha kuwa kuna suala la kubaka watoto.

Afisa wa tume hii,Jean Marie Vianney Makombe amewanyoshea kidole wachuuzi wadogo akisema kuwa wanapatia watoto fedha kisha wakafanya mapenzi nao.

Kwa upande wa wachuuzi wadogo wamekubali kuwa kuna suala hili la wachuuzi wanaofanya mapenzi na watoto.

Mmoja wao,Francois Ngendahayo ambaye ni mchuuzi mjini Ruhango,kusini mwa nchi amekubali kuwa baadhi yawachuuzi wanaojihusisha na maovu haya ya kufanya mapenzi na watoto.

Kuna wachuuzi wanaopatia waschana vitu vyenye utamu kama vile maandazi kisha wakafanya mapenzi nao”amesema Francois

Tume hii imetangaza haya wakati ambapo serikali ilitangaza kuwa waschana 17,000 walipachikwa mimba mwaka wa 2017.

Sheria za kuadhibu ya nchi,makala yake ya 190,inaeleza kwamba uhalifu wa kufanya mapenzi na mtoto kwa kutumia namna yoyote unadhibiwa kufungwa maisha jela.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top