kwamamaza 7

Tulipokewa kama maraisi- waimbaji kutoka Tanzania wakishukuru Polisi ya Rwanda

0

Waimbaji 125 wa Kwaya ‘Blessed Maria Theresa Ledochowska’ kutoka Mjini Dodoma, Tanzania wameshukuru Polisi ya Rwanda kwa mapokezi na ilivyowasindikiza kutoka mpaka wa Rusumo kufika Kigali.

Kwenye ziara yao wiki iliyopita tarehe 28 Juni mwaka huu, walitembelea Kwaya ya kikatoliki “Il est vivant kumaanisha ‘Mungu ni hai’ ya Mjini Kigali, jimbo la Remera kwa lengo la kuimarisha urafiki.

Wageni hao wamambia Gazeti la Bwiza.com kwamba walidhani ni marais kutokana na huduma waliyopatiwa na Polisi ya Rwanda (RNP).

Tuliwaza sisi ni maraisi

Mwenyekiti wa Kwaya na Paluki wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma, Mhe. Paul amesema ilichofanya polisi ya Rwanda kiliwafurisha mno.

“Tulifika Rusumo na mabasi matano. Polisi ilikuwepo ikatusindikiza. Kila tulikofika walikuwa wakitutafutia njia kutoka Rusumo kufika Kigali. Tulifika kwa kikao cha balozi wa nchi yetu baadaye tukaenda Kibeho kukiwa na gari la polisi mbele kwenda na kurudi mjini. Maana yake polisi ilituheshimu sana. Na mbele tuliwaza ndugu wa Il est vivant walilipa faranga kwa Polisi, lakini lahasha, hii Polisi ya Rwanda inajua mgeni ni mfalme kabisa” Paul amesema

Polisi ilivyolinda usalama wa magari ya Kwaya

Baada ya kumaliza ziara yao tarehe mosi Julai nchini Rwanda, kupitia mitandao ya kijamii wanatuma ujumbe wao kuwapongeza wananchi hasa Polisi ya Rwanda.

“Tunashukuru Polisi ya Rwanda, mlichangia kuikamilisha ratiba yetu ndani ya wakati.” Mmoja wao ameandika

Ujumbe wa mmoja mwa wageni

Hii ni desturi yetu-  afunguka SSP Ndushabandi

Pamoja na hayo, Bwiza.com imezungumza na Msemaji wa Polisi kwa wajibu wa Usalama wa barabarani, SSP JMV Ndushabandi kuhusu hili.

Hayo  ni tabia ya Polisi shujaa, RNP, kila mtu anayepokea wageni wengi kisha akajulisha Polisi, sisi tunajitayalisha kumpa huduma bila malipo.  Hapo huwa tunataka kutoa nafasi njiani ili wasichelewe. Inatubidi kuwasaidia na kuwapisha njiani. Jingine ni kuchungulia spidi yao barabarani, ili wasipate ajali”, SSP Ndushabandi amesema

Gari la Polisi ya Rwanda likiongoza magari ya Kwaya kutoka Tanzania

Urafiki wa kwaya hizo, unazidi miaka miwili. Barozi wa Tanzania nchini Rwanda, Ernest Jumbe Mangu amesisitiza umuhimu wa urafiki huu kwa kudai inaanzia kidini halafu utageuka wa mambo ya kiuchumi.

Omar Karegeya/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.