kwamamaza 7

Timu ya Rwanda yapoteza mchezo wake dhidi ya Uganda kwa pigo kubwa

0

Timu ya taifa ya soka ya Rwanda( amavubi) imepoteza mchezo wake dhidi ya Uganda (The Cranes) kwa kichapo cha mabao matatu kwa bila.

Mechi dhidi ya Rwanda na Uganda ilipigwa kwenye Uwanja wa St Mary Kitende Stadium mechi ambayo ilikuwa kwa ajili ya kuwania tiketi ya kushiriki michuano ya afrika ya mataifa kwa wachezaji wa nyumbani (CHAN).

Mnamo dakika 16 za mchezo mchezaji wa Uganda Muzamiru Mutyaba aliipatia Uganda goli la Kwanza kupitia penati.

Mshambuliaji Derrick Nsibambi aliipatia The Cranes goli la pili baada ya dakika kumi tu.

Wakati Rwanda ilipokuwa ikijaribu kusawazisha kwa kufanya mabadiliko, Derrick Nsibambi aliipatia Uganda goli la tatu hap dakika ya 49 ya mchezo

Kutoka hapo hakuna mabadiliko ya matokeo yaliyokuweko na hivyo mechi kumalizika tatu kwa bila.

Rwanda itakukuwa na kibarua kikubwa kwenye mechi ya marudiano kwa kuwa watakuwa wakitakiwa kuwashinda Uganda bao nne kwa bila ili waweze kupata tiketi ya kushiriki mashindano ya CHAN yatakayofanyika nchini Kenya mwaka ujao.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.