kwamamaza 7

Tetesi muhimu za Usajili wa soka zinazovuma magazeti

0

Wakati huu ambao ni kipindi cha usajili huku timu zikijiandaa kwa msimu ujao huwa zinafanya juu chini kujenga vikosi vyake kwa kuwaongeza mikataba wachezaji na hata kuwasajili wachezaji viungo wapya

Huku Bwiza.com inakutembeza magazeti mbali mbali ikikufafanulia soko la usajili na tetesi muhimu.

Baada ya Everton kukubaliana na Manchester United dau la pauni milioni 75 ambayo huenda ikapanda hadi milioni 90 inasemekana atafanya vipimo vya Afya Los Angeles ambako yuko likizo  na mwandani wake Pogba (Mirror)

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa aliyeonyesha kukasirishwa na ujumbe kutoka kwa Antonio Conte kumjulisha kwamba hayuko mipanga ya meneja Conte kwa sasa inasemekana yuko tayari kuwa na mazungumzo na meneja huu kwa ajili ya kuichezea timu hii msimu ujao ( The Sun)

Ikiwa Lukaku anajiandaa kujiunga na Manchester United ripoti sasa zasema amekamatwa na polisi mjini Los Angels kwa kuzua kelele inayoweza kuwa hatari kwa usalama, ripoti inaendelea kusema kwamba hakupelekwa kituo cha polisi ila tu ametolewa onyo (daily star)

Kiungo wa Roma , Antonio Rudger yuko tayari kujiunga na Chelsea bada ya wakala wake kukubaliana na Chesea juu ya Usajili( Daily Star)

Mchezaji wa Leister City inasemeka atapenda kujiunga na Arsenal kuliko timu ya La Liga  ya Uhispania Barcelona.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Alexis Sanchez amekataliwa na timu yake ya Arsenal kuihama kwenda Man City licha ya kwamba ameiambia Arsenal kuwa anataka kuondoka na kwenda Manchester City. Makubaliano yamefikiwa kati ya Sanchez na City kwa pauni milioni 46.5, lakini Arsenal wamekataa kumuuza kiungo huo kwa timu hasimu ya EPL, lakini huenda akaondoka bure mwisho wa msimu ujao (El Mercurio).

Mshambuliaji wa Man City Wilfried Bony anasakwa na timu nyingi za Uchina na Manchester City wanapanga kumwuuza kwa pauni milioni 14  mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast (Independent).

Ni hayo katika magazeti tusubiri ni usajili upi utafaulu.

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.