kwamamaza 7

Tanzania:Kesi  ya Ingabire Victoire aliyoishtaki serikali ya Rwanda kumfunga kinyume na sheria  yaendelea

0

Mahakama ya kutetea haki za binadamu barani Afrika imesikiliza maoni  ya washtakiwa na washtaki kwa mala ya mwisho kuhusu kesi ambayo Ingabire Victoire Umuhoza anaishtaki serikali ya Rwanda kumfunga karibu miaka nane  kinyume na sheria.

Mmoja mwa wanasheria wa Victoire Ingabire Me Caroline,asili ya Uholandi  amesema kuwa anayoshtakiwa mteja wao ni uong’o mtupu na kuwa serikali ya Rwanda hushtaki uhalifu wa kuwa na itikadi ya mauaj ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994  wapinzani wake.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mwanasheria wake mwingine,Me Gatera Gashabana ameleza kuwa uamuzi wa mahakama za nchini Rwanda  wa kumfunga jela Ingabire Victoire miaka 15 haukufuata misingi halali husika na mahakama.

Me Gatera Gashabana amesema”uamuzi wa makama za Rwanda haukua halali,kuna misingi ambayo haikufuatiliwa wakati ambayo inahusika na mahakama,sheria hazielezi vizuri vya kutosha,mtu anaweza kutoa hoja bila kujua kuwa ni uhalifu kulingana na sheria(…)”

[xyz-ihs snippet=”google”]

Taarifa za VOA zinasema kuwa Serikali  ya Rwanda haikuonekana mahakamani tangu kesi hii ilipoanza ila iliandika barua moja ikieleza kuwa haitakuja mahakamani kwa kuwa mahakama hii hupatia fursa wanaotuhumiwa kushiriki katika mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi,madai ambayo mkurugenzi wa mahakama hii alikanusha alipozungumza na VOA.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pamoja na haya,wanahaki za binadamu wakiwemo Me,Donald ambaye ni mkurugenzi wa majaji bara Afrika amesema kuwa Rwanda imepata hasara kwa kuwa ingekuja mahakamani na kutoa hoja zake.

Huyu ameongeza kuwa kutokuja kwake haitazuia kesi kuendelea kulingana na sheria na kuwa Rwanda haina budi kufuatilia uamuzi wa kesi hii.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mahakama itatoa uamuzi wake kuhusu kesi hii leo tarehe 24 Novemba 2017.

Ingabire Victoire alishtakiwa uhalifu wa kukanusha mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi,itikadi ya mauaji ya kimbali,kuungana na kundi la wanamgambo wa FDRL na kuunda kundi la wanamgambo.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.