kwamamaza 7

Tanzania:Ingabire Victoire ashinda kesi aliyoishtaki serikali ya Rwanda kumfunga kinyume na sheria

0

Mahakama ya kutetea haki za binadamu barani Afrika yenye makao mjini Arusha imeamua ushindi wake mwenyekiti wa chama cha upinzani FDU-Inkingi Ingabire Umuhoza Victoire kwenye kesi aliyoishtaki serikali ya Rwanda kumfunga kinyume na sheria.

Mahakama imeamua ushindi wa Victoire wakati ambapo serikali ya Rwanda haikuhudhuria kesi tangu ilipoanza mwaka 2014 ila iliandika barua ikieleza kuwa haitakuja mahakamani kwa kuwa mahakama hii hupatia fursa watuhumiwa wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994,jambo alilokana mno mkurugenzi wa mahakama hii alipozungumza na VOA.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pamoja na haya serikali ya Rwanda ilijiondoa katika mahakama hii na kukataa haki za watu binafsi ama mashilika kushtakia Mahakama hii.Hata hivyo,wagombaniaji wa haki za binadamu wakiwemo Me Donald ambaye ni mkurugenzi wa majaji barani Afrika wiki iliyopita alisema kuwa serikali ya Rwanda ingelikuwa vizuri kuja mahakamani ili kutoa hoja zake kwa kuwa itapaswa kutii uamuzi wa mahakama kuhusu kesi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Ingabire Umuhoza Victoire alihukumiwa kufungwa miaka 15 juu ya uhalifu wa kukanusha mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi,itikadi ya mauaji ya kimbali,kuungana na kundi la wanamgambo wa FDRL na kuunda kundi la wanamgambo.

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.